
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameungana na wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa ya jirani ya Kanda ya Ziwa katika zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo leo Machi 24, 2021.
Viongozi wengine wa Serikali pia wamefika Mwanza kuaga mwili wa Magufuli akiwemo aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dkt. Willbroad Slaa ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Sweeden.
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameungana na wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa ya jirani kuaga mwili wa Hayati Dk. John Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba.
Makonda aliyeondoka kwenye wadhifa huo baada ya kuomba kugombea ubunge Kigamboni ameonekana uwanjani hapo akiwa ameongozana na waombolezaji wengine akiwa amevalia kaunda suti nyeusi.
Kabla ya kuwa mkuu wa Mkoa, Makonda aliyeibukia kwenye uongozi wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) alikuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Baada ya Makonda kujitosa kuwania ubunge na kushika nafasi ya pili katika kura za maoni ndani ya CCM, Magufuli alimteua Aboubakar Kunenge kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwili wa Hayati Magufuli uatzikwa siku ya Ijumaa Machi 26, 2021 katika kijiji cha Mlimani kilicho katika Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita.