
Lithuania, Latvia na Estonia ambazo ni Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) zimeitaka Urusi kuruhusu kutolewa kwa huduma za Afya kwa mkosoaji wa Rais Vladimir Putin, Alexey Navalny.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hizo wameeleza hayo kufuatia ripoti za Afya ya Navalny wakisema huduma hiyo ni Haki ya Wafungwa. Pia wamezitaka Jamii za Kimataifa na Viongozi wa EU kupazia sauti suala hilo.
Wito wao umetolewa baada ya washirika wa Navalny kusema wanataka ushahidi kuwa ana Afya njema baada ya Wanasheria wake kuzuiwa kumuona. Mapema leo, Mamlaka ilisema hali ya Mwanasiasa huyo wa Upinzani ni ya kuridhisha.