×

New Zealand Yaruhusu Mapumziko kwa Wanaopoteza Watoto

Bunge la New Zealand limepitisha Sheria inayowapa Wanawake pamoja na wenza wao Haki ya kupewa mapumziko yenye malipo pale ujauzito unapotoka au Mama anapopoteza Mtoto kabla au wakati wa kujifungua.

Sheria hiyo iliyopitishwa Machi 24, 2021 inawezesha Mfanyakazi kupata mapumziko ya siku tatu ikiwa atapoteza Mtoto, na hatochukua siku hizo kutoka kwenye zile za mapumziko ya kuumwa.

Mbunge aliyeanzisha Muswada huo amesema itatoa fursa kwa Wanawake na wenza wao kukabiliana na hali ya kupoteza Mtoto pasipo kutumia mapumziko ya kuumwa, kwasababu majonzi yao sio Ugonjwa.

Leave a Comment