×

Spika Ndugai Amkaribisha Rais Samia Bungeni – Video

 

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemhakikishia Rais wa sita wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ushirikiano wa chombo hicho cha kutunga sheria na kumkaribisha bungeni jijini Dodoma.

 

 

Ndugai ameyasema hayo leo Ijumaa Machi 26, 2021 katika ibada ya kuaga mwili wa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Hayati John Magufuli katika uwanja wa Magufuli mjini Chato, Geita.

 

 

Amesema bungeni Dodoma palikuwa ni nyumbani kwake na alifanya kazi nyingi na kutoa fursa nyingi jambo ambalo Watanzania wanatakiwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa maisha ya Magufuli.

 

 

“Kipekee sisi Bunge tumhakikishie mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan ushirikiano wa kila aina tutasimama naye kwa kila ambalo tunaweza kufanya kuhakikisha kwamba anafanikiwa na nchi yetu inafanikiwa zaidi na zaidi.”

 

 

“Nitumie fursa hii kumkaribisha bungeni pale ndiyo anaweza kuzungumza na Watanzania wote kwa siku ambayo anaona yeye inafaa. Watanzania wote kwa kuwa leo ni ibada nikumbushe neno linatoka kitabu cha Isaya 41:10 Mungu anasema ‘usiogope kwa vile yeye Mungu yu pamoja nasi anatuambia tusifadhaike kwa maana yeye atatutia nguvu, anasema nitawasaidia nitawashika kwa mkono wangu wa kuume’,” amesema Ndugai.

 

 

Leave a Comment