×

LG Electronics Yafunga Biashara ya Utengenezaji Smartphone

Kampuni ya LG Electronics leo imesema itafunga Biashara yake ya utengenezaji wa simu janja ambayo kwa takriban miaka sita imepata hasara inayofikia Dola za Marekani Bilioni 4.5.

 

 

Kampuni hiyo ya Korea Kusini ambayo mwaka 2013 ilitajwa kuwa Kampuni kubwa ya tatu kwa utengenezaji wa simu janja imesema ushindani wa soko umekuwa mgumu.

 

 

Kwa mujibu wa taarifa ya LG, uamuzi wa kuachana na sekta hiyo utawezesha Kampuni kuelekeza rasilimali kwenye maeneo mengine yenye ukuaji yakiwemo ‘Smart Homes’ na ‘Artificial Intelligence.”

Leave a Comment