×

Bango la Wananchi Kuondoka na Mkurugenzi, DC – Video

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema viongozi wa kitaifa wakikutana na mabango katika ziara zao, atawaondoa kazini mkurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya husika.

 

 

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 6, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuwaapisha makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu aliowateua Aprili 4, 2021.

 

 

Amesema imekuwa ni kawaida viongozi wakifanya ziara mikoani na wilayani wanapokewa na mabango ya wananchi wakilalamikia kero mbalimbali na masuala wanayolalamikia si ya kitaifa.

 

 

“Tumezoea tunapokwenda kwenye ziara mikoani na wilayani tunapokelewa na mabango ya wananchi wakilalamika kero mbalimbali, mabango yale mengine wala siyo mambo au masuala ya kushughulikwa katika ngazi za juu ni masuala ya kushughulikwa huko chini.”

 

 

“Kwa hiyo naomba tunapokuja huko mimi na makamu wa rais, waziri mkuu tukikuta bango basi ziwe inshu ya kitaifa lakini siyo mambo ya kushughulikiwa kule chini, nataka niseme bango moja aidha mkurugenzi au mkuu wa wilaya amekwenda na hii haina maana mkazuie watu kuandika kero zao,” amesema Rais Samia.

 

 

Amesisitiza, “Kwa sababu najua tunapokuja watu wanakuja na mabango mbio mnakwenda kuyakusanya na kuwanyuka watu kuwapelekea mnapokujua nyie ili wasiseme yao yanayowasibu, naomba kero za wananchi zikashughulikiwe, tunapokuja na kukuta bango moja mkuu wa wilaya au mkurugenzi umekwenda na tukikuta malalamiko kwamba mnawafinya wananchi wasiseme hivyo hivyo tutashughulikiana.”

 

 

Mbali na hilo Rais Samia amewataka watendaji wa Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi.

 

 

“Upande wa Ardhi, watu wameporwa sana ardhi zao na wanaohusika kwenye uporaji ni watendaji wa taasisi wanahusika kutengenezea wezi nyaraka feki, acheni mara moja naomba hili likafanyiwe kazi,” – amesema Rais Samia Suluhu.
Kuhusu ukusanyaji wa mapato, Rais Samia ameitaka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwenda kukusanya mapato na matumizi yafanywe kwa kufuata sheria na kanuni zilizopo.

 

 

“Nimemleta waziri mwanamama madhubuti, nimempa katibu mkuu mzuri na wasaidizi ni imani yangu kwamba kazi itafanywa,” amesisitiza kiongozi huyo.

 

 

Ameitaka Tamisemi kwenda kuongeza usimamizi kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ili kazi ziende vizuri.

 

🔴#LIVE​​: RAIS SAMIA AWASHA MOTO, AWAAMBIA VIONGOZI – “NIKIKUTANA NA BANGO MOJA, DED, DC MNAONDOKA”

Leave a Comment