×

Rais Samia: Nitadumisha Mazuri Yaliyopita, Yaliyopo na Kuleta Mapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan analihutubia Taifa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma ikiwa ni Mara yake ya kwanza tangu aapishwe kuchukua madaraka ya Urais.

 

Akizungumza wakati wa hotuba yake, Rais Samia amesema; “Naomba nieleze Bunge hili tukufu pamoja na Watanzania kuwa dira na mwelekeo wa awamu ya sita itakuwa ni kudumisha mazuri ya awamu zilizopita, kuyaendeleza mema yaliyopo na kuleta mengine mapya.

 

 

“Kimsingi ndio dhana na maana halisi ya kauli mbiu au salamu yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi iendelee, tutaenzi na kuendeleza mambo yote mazuri lakini pia tutafanya mabadiliko pale itakapobidi kwa lengo la kukuza ufanisi na tija.

 

 

“Hatutakuwa tayari kuvumilia uvivu, uzembe na ubadhirifu wa mali au fedha za umma na kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuvutia zaidi wawekezaji. Tunalenga kuachana na uchungaji wa kuhama hama kwani hauna tija, katika miaka hii mitano tutawekeza katika kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa na kuongeza uzalishaji wa vyaula vya mifugo viwandani.

 

“Tunakusudia kuongeza maeneo ya ufugaji lengo likiwa ni kuepusha wafugaji kuhama hali inayopelekea uharibifu wa mazingira na migogoro ya ardhi Tunatarajia kununua meli nane za uvuvi ili zishiriki katika uvuvi wa bahari kuu, nne zitafanya kazi Zanzibar na nne zitafanya kazi Tanzania Bara,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake bungeni leo.

Leave a Comment