×

Rais Samia Aagiza Pesa za Muungano Zigawanywe Bara na Zanzibar

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha zilizotakiwa kutumika katika shughuli za Maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano zigawanywe pande hizo mbili.

 

Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo Jijini Dodoma katika Kongamano la Miaka 57 ya Muungano. Ameongeza, kila upande utaamua namna ya kutumia fedha hizo kwa shughuli za maendeleo.

 

Ameeleza, “Mwaka huu kutokana na tukio la hivi karibuni ambapo Nchi yetu iliondokewa na mmoja wa Mashujaa wake, Hayati Dkt. Magufuli, tuliamua badala ya Sherehe tuadhimishe Muungano kwa kuwa na Kongamano.”

Leave a Comment