
SERIKALI ya Kenya imesitisha kwa muda safari za ndege za abiria wanaotoka India. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la maambukizi ya Corona-kusini mwa Asia mwa taifa hilo.
Katazo hilo litaanza Jumamosi na kudumu kwa muda wa wiki mbili. Lakini ndege za mizigo zitaendelea kufanya kazi.
Mtu yeyote anayewasili kutoka India kabla ya hapo atapimwa virusi vya corona na wakikutwa na corona watalazimika kujitenga na kukaa karantini kwa gharama zao wenyewe.
Kwa sasa India inakabiliwa na janga kubwa la virusi vya corona. Hospitali zimelemewa kwa kuwa na wagonjwa wengi na ripoti za watu kufariki mitaani zikiongezeka.
Zaidi ya wagonjwa 350,000 wa virusi vya corona wameripotiwa ndani ya saa 24 zilizopita – na hii kuwa rekodi mpya ya dunia.
Mataifa ya Afrika yanategemea kupata chanjo kutoka India kwa kutumiwa mpango wa Covax . Ingawa ongezeko la maambukizi limesababishwa kupiga marufuku usafirishaji wa chanjo hizo na kuangazia watu wake kwanza.
Malawi imepiga marufuku pia wasafiri wanaotoka India, pamoja na Bangladesh, Brazil na Pakistan kutokana kusambaa kwa virusi vya corona katika hayo mataifa.