
Mbunge Florent Kyombo amesema wananchi wa Mkoa wa Kagera ambao unapakana na nchi tatu wamekuwa wahanga katika kutambuliwa na kupatiwa vitambulisho vya Taifa.
Amesema, “Wilaya za Kyerwa, Karagwe, Missenyi na Ngara wote tumekuwa Wahanga wa kukosa vitambulisho na Wananchi wanaishi kwa tabu kama vile hawapo ndani ya nchi yao.”
Akizungumzia Wilaya ya Missenyi Bungeni Mbunge huyo amesema, “Ukitaka kupima Mwananchi kwa kuongea Kiswahili na kuimba wimbo wa Taifa sisi wote sio Raia.”