
Mama mmoja anayejulikana kwa jina la Hidaya Mtaremwa mkazi wa kibada wilaya ya kigamboni Dar ea salaam amefunguka na kusema aliamua kuanzisha kituo Cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu ili kuenzi maisha yake ya utotoni.
Akizungumza na global TV online baada ya kutembelewa na Tasisi ya Jessy Foundation waliojitolea kusaidia baadhi ya mahitaji ya watoto hao Bi Hidaya amesema katika maisha yake ya utotoni alikua mtoto yatima na amelelewa na Bibi yake baada ya wazazi wake kufariki.

Bi Hidaya ameishukuru Tasisi ya Jessy Foundation Kwa Msaada huo na kuomba wadau wengine, Kampuni na Tasisi za Binafsi na serikali kuunga mkono juhudi zake ili aweze kusaidia watoto wengi zaidi.
Kwa upande wake Antony Mbutu ambaye ni mratibu wa mirabu wa mirasi wa Tasisi hiyo amesema lengo kubwa la kuanzisha Tasisi hiyo ni kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo watoto yatima, Wazee na.wenye mahitaji maalumu.
Kituo hicho kijulikancho kama Hisani Orphanage kipo Kibada wilaya ya kigamboni na kina jumla ya watoto 60 Hadi Sasa wenye umri kuanzia miaka miwili na kuendelea,