The House of Favourite Newspapers

Mourinho Atangazwa Kuwa Kocha Mpya wa AS Roma

0

Klabu ya AS Roma ya Italia imemtangaza Mourinho kuwa Kocha wake ikiwa ni wiki mbili tangu kibarua chake kiote nyasi akiwa Tottenham Hotspurs.

Mourinho (58) ambaye ni raia wa Ureno, amesaini kandarasi ya miaka mitatu na ataanza kuinoa AS Roma mwanzoni mwa msimu ujao.

Kocha huyo aliyewahi kufundisha Klabu za Porto, Chelsea, Real Madrid, Inter Milan na Manchester United, akiwa Tottenham alishinda michezo 45, kufungwa 24 na kutoka sare 17.

Leave A Reply