
MSHAMBULIAJI na Nahodha wa Simba, John Bocco anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Hiyo ni baada ya kupona majeraha yake ya enka yaliyomfanya aondolewe kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza dhidi ya DR Congo na Madagascar katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022.
Septemba 19, mwaka huu, Simba itavaana na TP Mazembe katika mechi ya kirafiki itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar kwenye Tamasha la Simba Day.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Simba, Abbas Ally, alisema: “Bocco yupo kambini, alikuwa nje ya uwanja kwa ajili ya matibabu ya haraka ili kuhakikisha anarejea uwanjani mapema.“Bocco amepona majeraha yake na leo (jana) asubuhi alianza mazoezi mepesi ya binafsi,” alisema Ally.
STORI: WILBERT MOLANDI, DAR