×

Mugalu, Bocco Wakabidhiwa Yanga

UNAAMBIWA Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, hataki kuvurugiwa rekodi na Yanga ambapo tayari ameikabidhi mechi hiyo kwa washambuliaji wake, John Bocco na Chris Mugalu.

 

Baada ya mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ambapo Yanga na Simba zilitoka sare ya bao 1-1, Jumamosi hii timu hizo zitakutana tena Uwanja wa Mkapa, Dar kusaka pointi tatu ambapo kwa sasa Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 61, huku Yanga ikishika nafasi ya pili ikikusanya pointi 57.

 

Kwenye mazoezi ya Simba yaliyofanyika juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Dar, Spoti Xtra lilimshuhudia Gomes muda mwingi akiwapa maelekezo ya kina Mugalu na Bocco namna ya kukaa na mpira wanapokuwa wanashambulia lango la wapinzani na kuwapa mbinu za kufunga.

Mfumo alioanza nao kwenye mazoezi hayo ulihusisha viungo washambuliaji ambapo kwenye timu ya Bocco alikuwepo Parfect Chikwende na Bernard Morrison, huku upande wa Mugalu akiwatumia Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin ambapo majukumu yao makubwa yalikuwa ni kutibua mipango ya wapinzani na kutoa pasi za mwisho kwa washambuliaji.

 

Viungo hao walipokuwa wakitoa pasi za mwisho kwa Mugalu na Bocco, Gomes alikuwa akiwasisitiza namna ya kutumia nafasi hizo kufunga mabao wakiona nafasi, lakini ikishindikana, basi wakae na mipira isipotee.

STORI: MUSA MATEJA NA JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave a Comment