
JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe, limemhoji Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Mbozi, Ignas Kinyowa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janneth Magomi ameyasema hayo jana Jumatatu Oktoba 4, 2021.
Mhe. Mwenisongole ambaye hivi karibuni alichomewa gari lake aina ya Brevis likiwa nyumbani kwake majira ya usiku ambapo alidai tukio hilo ni hila za kisiasa, anadaiwa kuwa ameshirikiana na wenzake 2 kumpiga na kumjeruhi katibu huyo wa UVCCM.