
STAA wa Bongo Fleva, Nurdin Bilali ‘Shetta’ anasema katika mapambano yake ya kutafuta njia ya kutoboa kimuziki, amewahi kuishi nyumbani kwa staa mkubwa na ikafika hatua akawa anamuoshea gari lake.
Akizungumzana Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Shetta anasema kuwa, alifanya kazi yoyote ilimradi kutengeneza mpenyo kwa msanii huyo ambaye alikuwa anatamba kwa kipindi hicho.
“Niliosha magari sana ya hapo nyuma ya msanii mwenzangu kipindi bado sijatoboa kimaisha. Unajua kwenye haya maisha hutakiwi kukata tama, huwezi kuamini, kuna kipindi nilikuwa hadi naitwa majina ya ajabu, lakini sikuwa nawasikiliza maana nilikuwa najua ninachokitafuta,” anasema Shetta ambaye kwa sasa anaishi maisha ya kifahari baada ya kufanya vizuri kwenye muziki wake.
STORI: KHADIJA BAKARI