
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo leo amezindua kampeni ya mafunzo ya ujasiriamali katika kisiwa Cha Kome Kijiji cha Ntama mafunzo hayo ambayo wanatolewa bure kwa wananchi wote wa Jimbo la Buchosa kwa kugharamikiwa na mbunge huyo.

Katika uzinduzi huo Shigongo amewaeleza wananchi wa Kijiji cha Ntama na Jimbo la Buchosa kwa ujumla dhamira yake ya kuwainua kichumi wananchi wa Buchosa aidha Shigongo amewataka wananchi wa Buchosa kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo ya kila mmoja na nchi kwa ujumla.


