×

Samia Atoa Onyo Ma-RC na Ma-RAS Wanawake: ‘Nisiisikie’ – Picha,Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Cpt. Mst. George Huruma Mkuchika kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum) katika hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo Juni 2, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ameteua asilimia 46 ya Makatibu Tawala Wanawake hivyo anataka kuona utofauti katika Utendaji badala ya kuendekeza majungu kazini.

 

Samia amesema hayo leo Jumatano, Juni 2, 2021 wakati akiwaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa na viongozi mbalimbali aliyowateua hivi karibuni, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kuwataka wawe watiifu kwa viongozi na wananchi.

Rais Samia akimuapisha Balozi Batilda Salha Burian kuwa Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga.

“Makatibu Tawala wa Mikoa mnakwenda kuwa watendaji wakuu wa mikoa, wakuu wa sekretarieti za mikoa na makatibu wa kamati za usalama za mkoa, mna kazi kubwa ya kwenda kufanya huko muendako, watendaji wote wa mikoa wako chini yenu.

 

“Nimewaweka wanawake asilimia 46 kwa maksudi, ninafahamu wanawake mna uwezo mkubwa wa kusimamia kazi. Tumeona walipokuwa Ma-RAS wengi wengi wanaume hawakufanya vizuri sana, sasa hivi mmekaribia kulingana, tunaamini nyie mtaweza, mkishindwa basi tena.

 

“Kwa mikoa ambayo kuna wanawake kwa wanawake, ile ‘Bibi usinibabaishe’ nisiisikie, pale nyinyi sio wanawake ni mkuu wa mkoa na RAS wako, hakuna sababu ya kuparurana, mkifanya hivyo mtaniabisha mimi, yakayosemwa ndio tabia za wanawake, mbona mnaolewa pamoja.

Rais Samia akimuapisha Rodrick Lazaro Mpogolo kuwa Katibu Tawala mkoa wa Katavi
Rais Samia akimuapisha Dorothy Aidan Mwaluko kuwa Katibu Tawala Singida.
Rais Samia akimuapisha Dkt. Athumani Juma Kihamia kuwa Katibu Tawala mkoa wa Arusha.
Rais Samia akimuapisha Mwanaasha Rajabu Tumbo kuwa Katibu Tawala mkoa wa Pwani
Rais Samia akimuapisha Ngusa Dismas Samike kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mwanza.
Rais Samia akimuapisha Hassan Abasi Rugwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam.
Rais Samia akimuapisha Fatuma Ramadhan Mganga kuwa Katibu Tawala mkoa wa Dodoma.
Rais Samia akimuapisha Musa Ramadhani Chogero kuwa Katibu Tawala mkoa wa Geita.
Rais Samia akimuapisha Pili Hassan Mnyema kuwa Katibu Tawala mkoa wa Tanga.
Rais Samia akimuapisha Prisca Joseph Kayombo kuwa Katibu Tawala mkoa wa Simiyu.
Viongozi mbalimbali walioapishwa pamoja na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mara baada ya tukio la Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

“Muende mkachape kazi wanawake kwa wanawake, hiyo mikoa naitegemea sana, nione impact ya kuweka wanawake pamoja, kazi ziende, spidi iende, nataka kuona hayo matokeo,” amesema Rais Samia.

 

Leave a Comment