×

Mkuchika: Aanika Alivyoagana na JPM Kabla ya Kifo ‘Niliugua Pingili’

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, George Mkuchika leo amerejea bungeni baada ya kukosekana kwa miezi mitatu huku akisema kauli ya mwisho aliyotamkiwa na hayati John Magufuli ni ‘nenda ukatibuwe ukirudi tuchape kazi.’

 

Mkuchika ambaye ameapishwa leo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu amesema kwa sasa amepona na yupo tayari kwa ajili ya kuchapa Kazi.

 

Mkongwe huyo amezungumza bungeni leo, Jumatano, Juni 2, 2021 wakati akiwasalimu wabunge baada ya kupewa nafasi na Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kwa miezi mitatu alikuwa nje ya nchi kwa matibabu.

 

“Sikuwa na Wabunge wenzangu karibu miezi mitatu, niwaambieni tatizo lililonipeleka nje limekwisha kabisa, ugonjwa wa Mtu kuugua pingili sio kama UKIMWI, Wataalamu wanapiga operesheni wanapanga upya lakini yenyewe iliua kabisa miguu yangu…” amesema Mkuchika.

 

Hata hivyo ameshukuru namna Katiba ya Tanzania ilivyo nzuri kwamba imewaongoza Watanzania kupata Rais mwingine baada ya kifo cha Magufuli kilichotokea Machi 17, mwaka huu na sasa kazi zinaendelea.

 

Akizungumzia majukumu yake, amesema Watanzania waamini anakwenda kufanya kazi ambayo ni maalumu itakayotokana na mwongozo wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Leave a Comment