
BEKI wa klabu ya Manchester City Ruben Dias ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu 2020/2021.
Dias ameshakusanya tuzo mbili mpaka sasa ile ya mchezaji bora wa mwaka wa waandishi wa habari za soka EPL (FWA Player of the year).
Na pia ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi kuu ya Uingereza (Premier League Player of the Year).
Na bado yupo katika orodha inayowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa soka la kulipwa inayopigiwa kura na wachezaji wa EPL (The Professional Footballers’ Association Men’s Players’ Player of the Year)
Dias ambaye alijiunga na city akitokea Benfica kwa ada ya uhamisho wa paundi mil. 65 amecheza mechi 32 za ligi, amefunga bao moja na kufanikiwa kupata clean sheet 15.
Mreno huyo amewashinda Kevin De Bruyne ambaye wanacheza timu moja ya city, na mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane.
Nyota huyo anatarajiwa kuiwakilisha Ureno kwenye michuano ya Uero 2020.