×

‘Grealish ni Ronaldo wa England’

JACK Grealish alikuwa ni Cristiano Ronaldo wa England katika mchezo wa Jumatano iliyopita walipocheza dhidi ya Austria, hiyo ni kwa mujibu wa Roy Keane.

 

England ilishinda bao 1-0 katika mchezo huo wa kirafiki na kushuhudiwa nyota huyo wa Aston Villa akionyesha uwezo wa juu. Keane ambaye anajulikana kwa kuwa mkosoaji kwa watu wengi katika soka, alimsifia Grealish kwa kuonyesha uwezo mkubwa.

 

“(Grealish) ni nyota, alitengeneza nafasi nyingi, amekuwa na ile tabia ya kuutaka mpira katika mazingira magumu.“Alikuwa kama Cristiano Ronaldo akiwa Ureno, unahitaji wachezaji wa aina hiyo katika timu,” alisema Keane.

Leave a Comment