×

Video: Afisa Wa Serikali Aiba Milioni 36 Na Kuacha Kazi Ghafla


Inaelezwa kuwa kwenye halimashauri ya meru kuna upotevu wa pesa ya serikali zaidi ya million 48 ambapo mtumishi mmoja wa serikali anatuhumiwa kukwapua kiasi cha chilingi milioni 36 na laki moja na 26 aliyotakiwa kuipeleka benki lakini hakufanya Hivo


Baada ya ukaguzi kufanyika kugundulika upotevu wa Fedha hizo Mtumishi huyo aliamua kuacha kazi ndani ya msaa 24 na kuanza kufatilia mafao yake ya kustaafu.

 

Taarifa yake imewasilishwa kwenye baraza la madiwani la halimashauri meru ambapo imeelezwa kuwa mtumishi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi wa Taasisi ya kupambana na Rushwa nchini Takukuru

 

Dkt Athumn Kihamia yeye ni katibu tawala wa mkoa wa Arusha ambae pia alimwakilisha mkuu wa mkoa john Mongela kwenye kikao hicho baada ya kusikia Taarifa hizo za upotevu wa fedha anatoa msimamo wa serikali juu ya Tabia hizo za baadhi watumishi wa uma wasiokuwa waadilifu.

Stori na Korumba Lebabazi

Leave a Comment