×

Willy Paul Avunja Ukimya kuhusu Muziki wa Injili

MWANAMUZIKI maarufu Willy Paul amevunja kimya chake kuhusu sababu iliyomfanya aache kufanya muziki wa injili licha ya nyimbo zake kuvuma na kupendwa na mashabiki.

 

Willy alifichua kwamba kuna watu wenye roho chafu katika sekta ya injili ambao walimnyanyasa na kufanya afilisike kiwango cha yeye kushindwa kumudu mahitaji yake.

 

” Umewahijiuliza ni kwa nini watu wanaweza kuchukia bila sababu? kuna maadui, wanatamani wangelikuwa na kile ulichonacho, wanatamani wangelikuwa wewe hata kwa robo ya sehemu yako,”  ni kipi sijakiona kwenye haya maisha? maisha ya ufukara, maisha matamu na ya kupendeza, wanawake warembo nakadhalika.

 

Watu wamenichukia bila sababu lakini sijakata tamaa, nitaendelea kufanya muziki kwa mujibu wa Willy, watu waliokuwa wakimpiga vita katika sekta ya injili ndio waliokuwa mstari wa mbele kumuuliza sababu ya yeye kuondoka katika muziki huo wa Injili.

Leave a Comment