
BADO muigizaji Irene Uwoya ameendelea kujadiliwa kwenye ulimwengu wa burudani na habari mpya ni kwamba, mwanaye Krish Ndikumana aliyepata Kumunio ya Kwanza Jumapili iliyopita amemponza na kujikuta akitukanywa.
Iko hivi, mara baada ya shughuli ya kanisani kumalizika, watu wamemvaa Uwoya kwa kitendo cha kumnyoa mtoto mtindo ambao si wa maadili na ukizingatia mtoto alipata sakramenti hiyo kanisani.
Wadau mbalimbali kwenye mitandao walimchana Uwoya kuwa, alipaswa kumuandaa vyema mwanaye kabla ya kumpeleka kanisani hata kama yeye ni msanii lakini asiufanye usanii kwa mtoto.

“Uwoya amekosea sana, unajua unapomlea mtoto kwenye maadili ya namna hii, atakapokuwa mkubwa ni rahisi kuharibika halafu ukaanza kulaumu,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.
Mdau mwingine anayefahamika kwa jina la Kioo, alisema Uwoya anapaswa kutofautisha maisha ya ustaa na mtoto maana atajikuta ametengeneza ‘bomu’ litakalokuja kumlipua yeye mwenyewe.“

Ukimlea mtoto kwenye mazingira ya ustaa ukasahau maadili, heshima na mambo mengine, baadaye utakuja kulaumu watu bure. Uwoya aangalie namna ambavyo anaweza kumwepusha mtoto kwenye ustaa,” alisema.
Mbali na hao, maoni mengi makali yalitupiwa na wadau mbalimbali ya kumtaka Uwoya awe makini asije akampoteza mtoto.
Kuna wadau wengine walienda mbali zaidi kwa kusema kama anaona ameshindwa kukaa naye basi ni vyema akampeleka akawa anaishi na mama yake (bibi wa Krish) ili mambo yasiwe mengi.
“Bora kama anaona vipi hata ampeleke kwa mama yake amlelee kuliko kumfanya mtoto kama toi,” alichangia mdau mwingine kwenye mtandao wa Instagram.
Krish ni mtoto pekee wa Uwoya aliyezaa na marehemu Hamad Ndikumana ambaye alikuwa staa wa mpira wa miguu kutoka pande za Rwanda.
STORI: MWANDISHI WETU, RISASI
BALAA JIPYA DIAMOND TUZO ZA BET, GIGY AMPONZA WEMA | HOT POT