×

Mwamba Wa Afrika Mpya Umeanguka

Ni nyakati nyingine mbaya kwa Bara la Afrika kwa kumpoteza mwamba mwingine ambaye alikuwa mmoja wa waasisi wa Afrika mpya, wakati nchi yake ilipoondokana na ukoloni na kuwa Taifa huru.

 

Alikuwa mmoja wa watu maarufu zaidi barani Afrika na mpiganiaji uhuru; Kenneth Kaunda, Rais wa Kwanza wa Zambia. Jana aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 97.

 

Mwaka 1950, Kaunda almaarufu kwa jina la KK, alikuwa mtu muhimu katika Vuguvu la kupigania uhuru wa Rhodesia ya Kaskazini (sasa Zambia) kutoka mikononi mwa ukoloni wa Waingereza.

 

Alikuwa Rais wa Kwanza wa Zambia mwaka tangu 1964 na kuongoza Taifa hilo kupitia miongo kadhaa ya utawala wa chama kimoja.

 

Alijiuzulu baada ya kupoteza katika uchaguzi wa vyama vingi 1991.

Kaunda alikuwa shabiki mkubwa wa juhudi za kumaliza ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

 

Alikuwa pia akiongoza mavuguvugu nchini Msumbiji na Zimbabwe.

Sasa Kaunda anaungana na majabali wengine wa Afrika waliotangulia mbele ya haki kama Nkwame Nkuruma, Nelson Mandela, Mwalimu Julius Nyerere, Robert Mugabe, Patrick Lumumba, Jomo Kenyatta na wengine wengi ambao wameacha alama isiyopfutika.

Stori na Sifael Paul

Leave a Comment