×

Rais Samia Awaapisha Viongozi Wawili

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu,Juni 21 2021 awaapisha viongozi wawili, hafla hiyo imefanyika katika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo Juni 21, 2021.

 

Aidha Rais Samia amemuapisha Balozi Batilda Buriani kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Kabla ya kuapishwa, alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga na amemuapisha Zuwena Omari Jiri kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.

Rais Samia alifanya mabadiliko hayo baada ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mara, Robert Gabriel.

 

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia alimhamisha mkuu wa mkoa wa Tabora, Ally Hapi kwenda mkoa wa Mara na kumteua Dk Buriani ambaye alikuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora huku nafasi yake ikichukuliwa na Jiri ambaye alikuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro.

 

Leave a Comment