×

Breaking: Bunge Lapitisha Bajeti ya Serikali Kwa Kishindo -Video

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Juni 22, 2021 limeikubali na kuipitisha bajeti ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

 

Spika Job Ndugai, ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma baada ya kukamilika kwa zoezi la kupiga kura na kueleza kuwa bajeti hiyo imepitishwa na asilimia 94 ya wabunge wote, kiasi ambacho ni kikubwa na hakijawahi kutokea katika siku za karibuni.

 

Ndugai amesema kati ya wabunge 385 walioipigia kura bajeti, hakuna kura ya hapana hata moja, na ni asilimia sita pekee ya wabunge walioshindwa kuamua huku wabunge watano wakiwa hawajahudhuria katika zoezi la kuipigia kura bajeti hiyo.

STORI NA AZIZ HASHIM | GPL

 

Leave a Comment