The House of Favourite Newspapers

Madai ya Aliyejifungua Watoto Kumi Sio ya Kweli

0

MAMLAKA ya mkoa wa Gauteng inasema kwamba wamefanya uchunguzi wa kina kubaini kwamba hakuna hospitali ya umma au ya kibinafsi ilioweka rekodi za kujifungua kwake.

 

Kulingana na mwandishi wa BBC Vumani Mkhize, hatua hiyo inajiri baada ya mwanamke huyo kudaiwa kujifungua Watoto kumi madai ambayo hayakuthibitishwa,Lakini hii leo mamlaka ya Gauteng imetamatisha sakati ya kisa hicho cha watoto 10.

 

Katika taarifa , idara ya afya inasema kwamba Gosiame Sithole hakujifungua hivi karibuni , na wala hakuwa na ujauzito wowote.

 

Taarifa hiyo hatahivyo haikueleza sababu za bi Sithole kubuni taarifa hiyo , lakini maafisa wa afya wamesema kwamba anapokea usaidizi wa kisaikolojia na ule wa kijamii.

 

Mwandishi aliyechapisha habari hiyo Piet Rampedi amejipata mashakani baada ya serikali kuagiza Ofisi ya mwanasheria mkuu kumfungulia mashtaka, Rampedi aliandika  habari akidai kwamba bi Sithole alijifungua Watoto 10 .

 

Ujauzito huo ulivutia hisia tofauti katika mitandao ya kijamii kote duniani na watu wakaanza kutuma ufadhili kwa wazazi wa Watoto hao.

 

Hatahivyo habari hiyo ilivutia shauku baada ya bwana Rampedi kushindwa kutaja hospitali ambayo watoto hao walizaliwa ,huku baadhi ya hospitali katika mkoa huo zikipinga madai kwamba mama huyo alikuwa amejifungua katika hospitali zao.

 

Shirika la habari la Mitandaoni Independent Online IOL, ambalo linamiliki Pretoria News na ambalo ndilo la kwanza kuripoti habari hiyo lilisimama kidete na kuunga mkono taarifa yake.

 

Siku ya Jumanne, taarifa iliovuja ilisema kwamba  Rampedi aliomba msamaha katika chombo cha habari cha Independent , akisema kwamba hiyo ilikuwa habari nzuri na kwamba alihisi hakuna haja ya kuyafanyia uchunguzi madai ya bi Sithole.

 

Meya wa eneo hilo baadaye alithibitisha kijifungua kwa mwanamke huyo na ni wakati huo ndiposa vyombo vingine vya habari ikiwemo BBC , vilichapisha habari hiyo – lakini msemaji wa serikali baadaye alisema kwamba mwanasiasa huyo aliwanukuu Bi Sithole na mume wake na kwamba hakuna aliyewaona watoto hao.

Michango ilianza kumiminika kwa wanandoa hao na watoto wao , waliopatiwa jina ”Thembisa 10” , ikiwemo $70,000; £50,000 kutoka kwa mwenyekiti wa IOL Iqbal Survé.

Lakini habari hiyo ilizua wasiwasi baada ya chombo cha habari cha Pretoria kushindwa kubaini hospitali ambayo watoto hao walizaliwa huku baadhi ya hospitali mkoani Gauteng zikijitenga na tukio hilo lisilo la kawaida.

Hata hivyo wanandoa hao walitofautiana baadaye huku bwana Tsotesti akiripoti kutoweka kwa bi Sithole na kuwawataka watu kutotuma michango yao wiki moja baadaye huku naye mwanamke huyo akisema kwamba bwana Tsotetsi alikuwa akitaka kujinufaisha kifedha kutoka kwa watoto hao, kilisema chombo cha habari cha Pretoria News.

 

Leave A Reply