×

Rais Ataka Kuvunja Ndoa ya Miaka 32

BAADA ya kuondolewa kesi na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Rais zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo amewasilisha kesi ya kutaka kuvunja ndoa yake ya miaka 32 na mkewe Simone.

 

Uhusiano wa Gbagbo na Simone umekuwa na doa na sasa kiongozi huyo inasemekana yupo mbioni kumuoa mwanahabari wa zamani.

Taarifa ya vyombo vya habari nchini humo ilieleza kuwa, Wakili wa Gbagbo alisema Rais huyo wa zamani ameamua kutengana na Simone baada ya zaidi ya miongo mitatu pamoja.

 

Taarifa hiyo inakuja siku chache baada ya Gbagbo kurejea Ivory Coast akitokea Mahakama ya ICC nchini Netherlands.

 

Gbagbo na Simone walikula kiapo cha ndoa mwaka 1989 kisha waliunda pamoja Chama cha Ivorian Popular Front ambacho kilishinda uchaguzi za mwaka 2000.

Leave a Comment