×

St. Marcus Schools Ilivyojipanga Kutoa Elimu Bora Tanzania

Miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika kutoa elimu bora na kuwaandaa wanafunzi katika kiwango cha juu kabisa, ni Shule za St Marcus, zilizopo Iwambi jijini Mbeya.

 

St. Marcus School ni mchanganyiko wa shule ya chekechekea, shule ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na cha tano hadi cha sita, ambapo kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita, michepuo inayofundishwa ni HGL, HGK na HKL.

 

Shule zote za St. Marcus zipo kwenye mandhari nzuri inayomfanya mwanafunzi awe na utulivu wa kiakili na kihisia, hivyo kumfanya aelewe kwa ufasaha kile anachofundishwa na ina mazingira bora yatakayomfanya mwanafunzi afurahie maisha yake ya kitaaluma awapo shuleni hapo.

Ubora wa elimu inayotolewa katika Shule za St Marcus, unadhihirika wazi kwenye matokeo ya mitihani ya taifa, kuanzia darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita ambapo kwa miaka yote tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ikifaulisha wanafunzi kwa kiwango cha juu kabisa.

 

Katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2020 kwa shule zenye zaidi ya wanafunzi 40 kwa darasa, Shule ya Msingi St Marcus, iliibuka kidedea na kushika nafasi ya kwanza katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, nafasi ya tatu kimkoa kati ya shule 461 na nafasi ya 54 kitaifa, kati ya shule 10659, ikitoa wanafunzi 42 waliopata Daraja A na wawili tu waliopata Daraja B.

 

Katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2020, Shule ya Secondari ya St Marcus, ilishika nafasi ya 7 kimkoa kati ya shule 176 na kutoa wanafunzi 16 waliopata Daraja la Kwanza (Division One), wanafunzi 25 waliopata Daraja la Pili (Division Two) na wanafunzi wanne tu waliopata Daraja la Tatu (Division Three).

 

Matokeo hayo ni ushahidi wa jinsi shule hiyo inavyotoa elimu yenye ubora, inayomuwezesha mwanafunzi kufaulu kwa kiwango cha juu na kumuandaa vyema kwa ajili ya masomo ya ngazi za juu zaidi ikiwemo kupata sifa za kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi.

 

Wakati muhula wa pili ukikaribia kuanza, uongozi wa Shule za St Marcus, unawatangazia wazazi, walezi na wanafunzi nafasi za masomo kuanzia ngazi ya chini kabisa, chekechekea, shule ya msingi na sekondari huku pia kukiwa na nafasi kwa kidato cha tano kwa michepuo ya HGL, HGK na HKL kwa wanafunzi wa bweni pekee.
Uzuri ni kwamba, ST Marcus School zinatoa elimu bora kwa ada nafuu kabisa, huku mzazi au mlezi akipewa nafasi ya kulipa ada taratibu mpaka kwa awamu nne kwa mwaka.

 

Ikiwa na Kauli Mbiu (School Motto) ya Quality Education for Brighter Future, St Marcus Schools ni sehemu sahihi kabisa ya kumpatia mwanafunzi elimu bora na kumfanya aje kuwa na maisha mazuri baadaye.
Kwa mawasiliano zaidi, piga simu namba 0754691038, 0758 420531 au 0755211507 au tembelea tovuti yao kwa kubofya www.stmarcusschools.ac.tz.

Leave a Comment