×

Jaji Mkuu Awapokea Mawakili Wapya wa Kujitegemea 308

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis (katikati) meza kuu katika hafla hiyo ya kuwa kuwapokea na kuwakubali Mawakili wapya wa Kujitegemea 308. 
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika hafla hiyo.
Sehemu ya mawakili wapya wa kujitegemea iliyokuwa imeandaliwa.
Mawakili wapya wa Kujitegemea 308 wakisikiliza hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis (hayupo pichani) iliyokuwa ikitolewa.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo Julai 09, 2021 amewapokea na kuwakubali Mawakili wapya wa Kujitegemea 308 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Idadi hii ya Mawakili wapya wa kujitegemea inaongeza idadi na kuwa na jumla ya Mawakili wa Kujitegemea 10,436 nchini.

Leave a Comment