×

Moto Kariakoo: Kamati Yaundwa Na Mkuu Wa Mkoa Dar -Video


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiwa soko kuu la Kariakoo, amesema serikali imeunda tume ya watu kumi kuchunguza na kupata ukweli wa chanzo cha moto na athari zilizopatikana ikiwemo mali zilizoteketea, pia amesema Waziri mkuu yuko njiani kuja kukagua na kuongea na wafanyabiashara na umma kwa ujumla.


Makalla amesema kamati itakuja na mapendekezo ya namna bora ya kufanya ili kuendelea kukabiliana na majanga ya aina hiyo.

Mkuu wa Mkoa amewaomba waathirika kuwa watulivu wakati Serikali inachukua hatua za kubaini chanzo na athari. Pia amewakaribisha Bima kuja kuona wateja wao (Ambao walikuwa wamekata bima).

Mkuu wa mkoa ameunda timu ya uchunguzi lakini bado haitoshi, hili soko ni la kimataifa. Itakuja timu ya kitaifa ambayo itaungana na timu ya mkuu wa mkoa.

Timu ya mkuu wa mkoa ni wale ambao walikuwa hapa kuanzia jana wakafanya kazi ya uokoaji na kusikia hiki na kile na kupata taarifa

Timu hii ya kitaifa kuchunguza moto itajumuisha wafuatao

  1. Ofisi ya RAS
  2. Ofisi ya Rais Ikulu na TAMISEMI
  3. Ofisi ya waziri mkuu-Mkurugenzi wa Maafa
  4. Vyombo vya ulinzi na usalama vinne(JWTZ, Polisi)
  5. TBA(Mhandisi wa majengo na Mhandisi wa umeme kwenye majengo)
  6. TANESCO
  7. Mwanasheria Mkuu
  8. Mkurugenzi wa Mashtaka

Leave a Comment