×

Simba Yaikalisha Coastal Union, Yatangaza Ubingwa

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba, imefanikiwa kutetea ubingwa wa ligi hiyo, baada ya kuitungua Coastal Union ya Tanga kwa mabao 2-0 mchezo ulipigwa jana Usiku Julai 11, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

 

Magoli ya Simba yalifungwa na Nahodha John Bocco dakika 13 na likiwa na bao lake na 15 akimzidi Prince Dube wa Azam mwenye magoli 14.

 

Goli la pili la Simba limekwamishwa na Chris Mugalu dakika ya 23 ya mchezo baada ya kumlamba chenga mlinda mlango wa Coastal Union.

 

Sasa ni rasmi Simba imetangaza Ubingwa baada ya kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, ikiwa bado na mechi mbili mkononi.

 

Huu ni Ubingwa wa wa Nne mfululizo kwa Mnyama Simba ambapo itapata fursa ya kuiwakilisha Taifa kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika.

Leave a Comment