×

Radi Yaua Watu 11 Wakijipiga Selfie

WATU takribani 11 wamefariki dunia hapo jana Kaskazini mwa nchi ya India baada ya kupigwa na radi wakati wakijipiga picha (Selfie) kwenye mvua wakiwa juu ya jengo eneo ambalo ni maarufu na ni kivutio cha utalii.

 

Watu 27 waliokuwepo katika jengo baadhi yao walidaiwa kujirusha chini, ambapo Afisa Mkuu wa Polisi aliviambia vyombo vya habari kuwa watu wengi waliouawa kwa radi katika jengo hilo walikuwa vijana.

 

Imeelezwa kuwa radi huuwa watu wapatao 2,000 nchini India kwa wastani kila mwaka, ambapo kwa siku ya Jumapili peke yake, wameshuhudia zaidi ya vifo tisa vikiripotiwa katika jimbo la Rajasthan ambako Jaipur ipo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

 

Kiongozi wa jimbo hilo, Ashok Gehlot, ametangaza kutoa kiasi cha dola 6,700 sawa na fedha ya India 500,000 rupees kama fidia kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Leave a Comment