×

Makamu wa Rais Zanzibar Afunga Maonyesho ya Sabasaba – Video

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah leo Julai 13, 2021, amefunga rasmi maonyesho ya Sabasaba katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Kilwa Road, Temeke jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza wakati wa kufunga maonyesho hayo na kukabidhi tuzo kwa washindi wa maonyesho na wadhamini, Mhe. Hemed amesema; “Kwa niaba ya Wazanzibari tunawapa pole Watanzania wenzetu kwa kuunguliwa na mali zao kwenye soko la Kariakoo, ninaupongeza uongozi wa Mkoa chini ya RC Amos Makalla kwa namna wanavyolishughulikia tatizo hilo.

 

“Ninaamini maonyesho haya yametoa fursa mbalimbali ya kujifunza kuhusu teknolojia, vifungashio na ubora wa bidhaa, yakawe chachu kwa wafanyabiashara waliopo chini kuboresha bidhaa na kukuza viwanda vyao.

 

“Tunao uwezo wa kupeleka bidhaa za Tanzania kwenye maonyesho ya biashara Dubai, kikubwa ni kujipanga na kusimamaia masoko haya, wafanyabiashara na wajasiriamali wetu waweze kukidhi matihaji hayo bila matatizo yoyote,”  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah.

 

Leave a Comment