×

Rais Samia Asimulia Umahiri Wa Hayati Mkapa -Video


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ashiriki Katika Kongamano la Kumbukizi ya Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Rais Benjamin William Mkapa.

 

“Hayati Mzee Mkapa alitoa fursa zaidi kwa Sekta Binafsi na kukaribisha uwekezaji kutoka nje. Hatua hizi zilisaidia kuongeza mapato ya Serikali kutoka TSH Bilioni 331.2 kwa mwaka 1995 hadi kufikia TSH Trilioni 2 kwa mwaka 2005”

“Mzee Mkapa alifanikiwa kupunguza Deni la Taifa kutoka 143.7 % ya pato la Taifa tulilokuwa tukidaiwa mwaka 1995 hadi 60.7% mwaka 2005 na hii ni baada ya Mzee Mkapa kuzishawishi Nchi Wahisani na Taasisi za Kifedha za Kimataifa kutusamehe madeni”

“Hii iliwezekana baada ya kutumia uwezo wake wa diplomasia kuzishawishi taasisi za kifedha za kimataifa na nchi wahisani kusamehe madeni kutumia mpango wa HIPC (Heavily Indebted Poor Countries) uliosimamiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la IMF”

“Mzee Mkapa alifanikiwa kupunguza deni la taifa kutoka 143.7% tuliyokuwa tukidaiwa mwaka 1995 hadi 60.7% mwaka 2005”

“Mzee Mkapa alianzisha taasisi nyingi ikiwemo TRA, PCCCB, TASAF, NHIF, TANROADS, Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC), Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), MKURABITA, Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na nyingine nyingi”
“Sifa nyingine ya Mzee Mkapa ni uwezo wake mkubwa wa kutokuogopa mijadala ya kimataifa, miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000 kulikuwa na vuguvugu la kupinga masuala ya utandawazi, yeye hakufuata mkumbo badala yake alijitokeza hadharani kuutetea”
“Serikali tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na Covid-19, ambapo kwa sasa tunakamilisha taratibu za kuagiza chanjo kwa ajili ya kinga, mwelekeo ni kwamba kila atakaye hitaji huduma ya chanjo iwe inapatikana, Chanjo hiyo ni yahiari” amesema Rais Samia.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment