Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitotoa maelezo juu ya malalamiko yaliyopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa na wabunge wa viti maalum 19 kuhusu kufukuzwa uwanachama baadala yake maelezo yote yatapelekwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu wa chama hicho.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila leo Julai 14, 2021 amesema mnamo tarehe 6/07/2021 walipokea barua kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa yakuwataka kuwasilisha maelezo juu yamalalamiko yalipolekwa ya kutokubaliana na tamko la chama la kuwafukuza wanachama.
“Kama kuna maelezo ambayo yapo ya kueleza kwa nini walifukuzwa, yatapelekwa kwenye Baraza Kuu kwenye rufaa, hayatapelekwa kwa Msajili kwa kuwa sio chombo cha rufaa wala Mahakama, hatuwezi peleka maelezo kwake,” amesema Bw. Kigaila.
CHADEMA kimeombwa kuletewa barua za waliolalamika ili wajibiwe “Lete barua zao waliolalamika ili tuwajibu hao, hawa wanaosema wanamlalamikia wanajua wanarufaa kwenye baraza kuu unapelekaje rufaa nyingine kwa Msajili huwezi kuwa na kesi moja kwenye Mahakama mbili tofauti,” amesema Bw Kigaila.
Mnamo tarehe 27 Novemba 2020 Chama cha CHADEMA kilimfukuzu Halima Mdee na wenzake kumi na nane uanachama kufutaia hatua ya kukubali kuapishwa kuwa wabunge viti maalum bila idhini ya chama chao.
