Dodoma: Julai 16, 2021: Wakati mashindano ya michezo mbalimbali ya majeshi yanatarajiwa kuanzaAgosti 4 mwaka huu jijini Dodoma, benki ya NBC limetoa msaada wa vifaa vyamichezo kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ili kusapoti jitihada za jeshi hilokatika sekta michezo.
Vifaahivyo zikiwamo viatu vya michezo, mipira, jezi pamoja na vifaa vingine vyamichezo mbalimbali vilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa michezo Kanda ya Ngome,Kanali David Mziray, na Meneja wa NBC tawi la Dodoma, Bi Happiness Kizigira.
Akizungumzabaada ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Kanali Mziray alisema vitasaidia kuongezahamasa kwa wachezaji wa timu za JWTZ ambao wamepania kuchukua vikombembalimbali vya mashindano hayo.
“Kupatakwa vifaa hivi kutawasaidia wachezaji wetu kuongeza hamasa zaidi kwenyemashindano hayo ambayo timu zetu zimepania kunyakua makombe yote,” alisemaMziray.
Menejawa NBC tawi la Dodoma Bi Happiness Kizigira akizungumza baada ya kukabidhivifaa hivyo, alisema wametoa vifaa hivyo kutokana na kuwapo na Ushirikiano katiya benki hiyo na jeshi la wananchi.
“Benkiya NBC tumekuwa na mahusiano mazuri ya muda mrefu na Jeshi la Wananchi na kwakuwa mwezi ujao wenzetu watakuwa na jambo lao hapa Dodoma ambalo kimsingitunawaombea mafanikio sana tumeona ni vema tuwaunge mkono ili mambo yaende vizuri zaidi,’’ alisema Kizigira.
Kizigiraalisema vifaa hivyo wamevitoa Makao Makuu ya Jeshi kwa lengo la kuwezakuwafikia wanamichezo wote wa jeshi hilo ambao watashiriki mashindano hayomwaka huu.