×

Video: Simba Yakabidhiwa Ubingwa wa VPL, Yainyuka Namungo 4-0

TIMU ya Simba imemaliza Ligi Kuu Tanzania Bara kibabe kwa kuitandika Namungo kwa mabao 4-0 kwenye mchezo wao wa mwisho wa msimu katika Dimba la Mkapa jijini Dar katika mechi ambayo imepigwa leo Julai 18.

 

Mabao ya Simba yamewekwa kambani na washambuliaji wake mahiri, Medie Kagere,dakika ya 19′ Chriss Mugalu aliyefunga mawili dakika ya 25′ na 66′ na John Bocco aliyefunga bao la penalti dakika 90+4.

 

Baada ya mechi hiyo, Simba wamekabidhiwa rasmi kombe lao la ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya nne mfululizo ambapo shangwe zimetawala uwanjani hapo.

Leave a Comment