WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa siku 90 kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wakala wa umeme vijijini (REA) kuanza mchakato wa kupeleka umeme wa gridi ya Taifa kwenye kisiwa cha Maisome ili kuwaondolea adha wanayoipata wananchi hao.
Kisiwa cha Maisome kina wakazi wapatao 20,000 kinachoundwa na vijiji vitatu vya Kanoni, Kisaba pamoja na Busikimbi kinapata umeme wa jua unazaolishwa na kampuni ya JUMEME ambao umekuwa ukilalamikiwa na wananchi kwa kutozwa bei ya Sh 2400 kwa uniti.
Dkt. Kalemani ametoa maagizo hayo jana Julai 18, alipotembea kisiwa cha Maisome kumaliza kero ya Wananchi walikuwa wakilalamikia kuuziwa Bei kubwa ya umeme kwa unit moja Sh 2400.
Licha ya kutoa maagizo kwa Tanesco kupeleka umeme wa gridi ya Taifa ametoa bei ilekezi ya Serikali kwa wananchi wanaotumia umeme wa jua unazaolishwa na kampuni JUMEME kuwa watakuwa wanauziwa uniti moja kwa Tsh 100 na siyo Tsh 2400 kama ilivyolivyokuwa awali.
“Nimetoa maelekezo ya Serikali hii ni kwa nchi nzima umeme wowote mwananchi auziwe kwa unit Moja Tsh 100 na maelekezo haya yasibadilike” amsema Kalemani.
Mmoja wa Wananchi wa kisiwa cha Maisome Elias Shikano amefurahushwa na maauzi ya Waziri ya kuwasidia kupunguza bei ya umeme hadi kumzawadi jadi la maji na kikombe vyote vilivyoko kwa kutumia mti.
Meneja mradi wa Kampuni ya Jumeme, Rwegasira Zadock ameseme wamepokea maelekezo ya Serikali na wao Kama kampuni watayafuata na kuwaondolea kelo Wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo amemshuru wa Waziri wa Nishati, Dkt. Merdadi Kalemani kwa kumaliza tatizo hilo ambalo lilikuwa kero kwa Wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ganga ameahidi kufuatia endapo kama maagizo ya Serikali yatapuuzwa na Wamiliki wa kampuni ya Jumeme kuendelea kutumia being ya zamani ya sh2400 kwa unit Moja.
Kisiwa Cha Maisome kimeingia kwenye historia mpya baada wa Waziri Kalemani kutoa maagizo kwa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kumia siku 90 wawe wamepeleka umeme wa gridi ya Taifa kwenye kisiwa hicho.




