×

Vodacom Yahitimisha Twende Mjini na M-Pesa Mdada Akiondoka na Ndinga Mpyaa

Neema akiwa na tabasamu kwenye ndinga yake.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imehitimisha promosheni yake ya Twende Mjini na M-Pesa iliyochukua wiki nane kwa kuwakabidhi wateja zawadi zao huku mdada Neema Ikolo wa Dar akiibuka na ndinga mpya kabisa aina ya Toyota Cluiz toleo la 2021.

 

Neema akiondoka na gari hilo, Sharifa Omary Kisaraza wa Karakata Dar ameondoka Bajaj mpya aina ya TVS. Wateja wengine wanne kila mmoja aliondoka na bodaboda mpya kabisa baada ya kujishindia kwenye promosheni hiyo.

 

Washindi hao wa bodaboda hizo  ni Asia Saidi wa Bagamoyo Pwani, Abdul Msumi Abbas wa Chanika Dar, Everline Baronga Richard wa Kariakoo Dar, Adelmas Kessy Paul wa Kibaha Pwani na Mariam  Kisaraza Salim wa Sinza Dar.

 

Akizungumz kwenye halfa hiyo baada ya ya kuwakabidhi zawadi washindi Mkuu wa Vodacom Kanda ya Dar na Pwani, Brigita Steven amesema amejisikia furaha kubwa sana kumkabidhi zawadi ya gari hilo jipya kabisa mshindi huyo pamoja na washindi wenzake.

Brigita amewataka watumiaji wote wa simu kutumia mtandao wa Vodacom ambao ni mtandao bora ambao kwasasa karibu minara yao yote ni ya 4G kwa ajili ya kuboresha kasi ya mtandao huo unaoongoza hapa nchini.

 

Naye Mkuu wa Mipango na Mikakati wa Vodacom, Nerusigwe Mwangota akizungumza kwenye hafla hiyo baada ya kuwapongeza washindi hao aliwataka watumiaji wengine wa simu kuchagua mtandao wa Vodacom na watumie huduma zao za M-Pesa ambazo zitawawezesha kufanya miamala yao kiurahisi.

 

Nerusigwe alisema ukitumia Vodacom utaweza kunufaika na mambo  mbalimbali ikiwemo huduma songesha inayoweza kumfanya mteja kuweza kukopa pesa kiwango anachotaka.

 

Nerusigwe amesema huduma nyingine ni pamoja na Voda Bima inayomuwezesha mteja kupata bima ya afya yake au ulinzi wa mali zake.

Leave a Comment