
MJANE wa aliyekuwa kiongozi wa Kundi la ToT, Hayati John Komba, Bi Salome Komba baada ya kifo cha memewe sasa ameamua kujiingiza kwenye ujasiriamali kwa kushughulisha na mambo mbalimbali ambapo wikiendi iliyopita amezindua ukumbi wa kisasa kabisa ambao ni kwa ajili ya sherehe na mikutano mbalimbali.

Akizungumza na wanahabari wetu Mama Salome Komba amesema aliamua kujenga ukumbi wa kisasa unaoitwa Salome Social Hall kama kumbukumbu ya mumewe ambaye alimshauri kufanya hivyo siku chache kabla ya kifo chake.

Akiuelezea ukumbi huo uliopo Mbezi Tangi Bovu kwenye kituo cha daladala cha Kwa Komba, Mama Salome amewakaribisha wadau mbalimbali ikiwemo waliokuwa mashabiki wa marehemu mumewe kumuendi kwa kwenda kukodi ukumbi huo.

Amesema kwa wanaohitaji kupatiwa huduma ya mapambo, keki, vinywaji na vya vyakula vyote vinapatikana ukumbini hapo.

“Nimeona nijiongeze maana nitakaa chini na kujiita mjane mpaka lini na pia sehemu ya mapato ninayopata kwenye biashara hii naitumia kwenda kuwasaidia wajane wenzangu, watu wenye uhitaji maalum na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali.
Nawaomba na wajane wenzangu waache kukaa chini na kuendelea kujiita wajane wapambane katika ujasiriamali ili maisha mengine yaendelee”, amesema Mama Salome.
Mama Salome amewataka wadau wanaotaka kumuunga mkono kwenye ukumbi huo kutumia namba ya mawasiliano 0752345234 au kufika eneo hilo.