×

Msimu Mpya Wa Shayiri, Neema Kwa Wakulima

Mkuu wa Wilaya Bi Janeth Mayanja amezindua msimu wa mavuno wa zao la shayiri katika kata ya Nangwa Wilaya ya Hanang.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa vyama vya ushirika vyote kutoka kata 33,Maafisa kilimo,Wadau wa maendeleo ya kilimo YARA Tanzania, TBL,CRDB, TADB, uongozi wa kata ya Nangwa na wakulima wa zao la shayiri.
Bi Janeth Mayanja ameeleza kuwa Wilaya hiyo Mungu ameipa upendeleo kwani udongo wake na hali ya hewa unafanya Wilaya ya Hanang kua kinara kwa uzalishaji wa shayiri jambo ambalo la upekee ukilinganisha na maeneo mengi nchini na amewakikishia wakulima uwepo wa soko la uhakika la zao la shayiri ambayo ni kampuni ya TBL ambao kutokana na upekee huo TBL wameamua kuingia kilimo cha mkataba.
Hivyo amewahimiza wananchi wa Wilaya ya Hanang msimu unaokuja wa mwaka 2022 kuongeza uzalishaji wa zao hilo na tija kwani soko la zao hilo ni la uhakika.Mkuu wa Wilaya ameomba mashirikiano zaidi na wadau wa maendeleo ya kilimo cha zao hilo ili kuongeza uzalishaji msimu wa Mwaka 2022.
Pia amewashukuru Benki ya kilimo (TADB), Kampuni ya YARA Tanzania,TBL kwa kuwasaidia wakulima wa za la shayiri na mazao mengine ya biashara na amewaahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali ili kuwasaidia wakulima wa zao la shayiri katika Wilaya hiyo.

Leave a Comment