×

Yanga Wamtambulishwa Heritier Makambo 

DILI la usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Horoya AC ya Guinea, Heritier Makambo limekamilika ambapo leo Agosti 3, 2021 ametabulishwa rasmi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

 

Makambo ni kati ya wachezaji waliokuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Yanga katika usajili wa msimu huu katika kuisuka safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

 

Makambo alikuwa katika mipango ya muda mrefu na uongozi wa Yanga tangu  msimu uliopita, lakini ikashindikana kutua kutokana na kubanwa na mkataba ambapo sasa amekuwa huru kutua Yanga baada ya kuachana na Horoya.

Leave a Comment