
JUMUIYA ya Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam Academic Staff Assembly) – UDASA inatangaza kifo Profesa Aloyce Mayo ambaye alikuwa mtumishi wa chuo hicho aliyefariki dunia usiku wa jana Jumatatu, Agosti 2, 2021, katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Licha ya kukitumikia chuo hicho, Prof. Mayo alikuwa mmiliki wa Shule za Alpha zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
