×

Prodyuza Mmarekani Kumchezesha Filamu na Ally Kiba

Prudyuza maarufu kutoka nchini Marekani,Tameko Tarnez ambaye amewahi kufanya kazi na marehemu, Michael Jackson, Bob Marley na wasanii mbalimbali,amekuja nchini Tanzania, kwaajili ya kufanya usajili kwa wasanii,ambapo mshindi atapata shilingi milioni 11 na tayari anatarajiwa kufanya kazi na msanii wa kizazi kipya Rosa Ree na yuko kwenye mazungumzo na Ally Kiba,pia kwaajili ya kucheza filamu ambayo ameiandaa.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Hotel ya Hayyat,iliyopo Posta jijini Dar amesema kuwa amekuwa nyuma ya kamera muda mrefu, sasa ameamua kuvunja ukimya na kuamua kujitokeza na kuonyesha uhalisia wake, na si kwenye uprodyuza tu, hata kwenye sanaa nyingine.

Leave a Comment