
KATIKA kuzidi kujiweka sawa na kujitengenezea nafasi nzuri Ligi Kuu Bara, uongozi wa Mtibwa Sugar umemshukia mshambuliaji wa Yanga, Wazir Junior ambaye alisajiliwa Jangwani msimu huu akitokea Mbao na kuishia kufunga mabao mawili tu kwenye ligi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Mtibwa, David Chitty Bgoya, amesema: “Ni kweli sisi tunamhitaji kama Yanga wakikubali kumtoa kwa mkopo, kwa sasa tunaelekea kwenye vikao vya usajili kujua nani tutamhitaji ili kuisaidia timu yetu kuwa kwenye nafasi nzuri msimu ujao.”
Stori: CAREEN OSCAR, Dar es Salaam