
Rasmi aliyekuwa nahodha wa timu ya Barcelona, Lionel Messi sasa ni mali ya PSG ya Ufaransa. Nyota huyo ambaye amedumu kwa muda wa miaka 21 ndani ya Barcelona amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru.
Ndani ya PSG, Messi amekabidhiwa jezi namba 30, namba ambayo alianza nayo maisha yake ya soka wakati akiwa ‘Nou Camp’ Barcelona.

Kwa ufupi historia ya Messi Barcelona
Messi ameshinda mataji 35 Barcelona alikodumu kwa miaka 21 tangu awasili akiwa na umri wa miaka 15 na akacheza mechi yake ya kwanza timu ya wakubwa mwaka 2004 alipofikisha miaka 16.
Kwa ujumla amecheza mechi 778 na kuweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwa mabao yake 672, yakiwemo 120 ya kwenye Ligi ya Mabingwa na 474 ya rekodi kwenye LaLiga.
Pia ameshinda mataji 10 ya LaLiga, manne ya Ligi ya Mabingwa na saba ya Kombe la Mfalme.
