×

Mifumo Mitatu Itakayoibeba Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi ashindwe mwenyewe katika msimu ujao ni kutokana na usajili ambao umefanywa hadi hivi sasa katika kila nafasi.

 

Hiyo ni katika kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la FA walilolikosa kwa misimu minne pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika watakayoshiriki msimu huu.

 

Yanga hadi hivi sasa imefanikisha usajili wa wachezaji nane ambao ni kipa raia wa Mali, Djigui Diarra, Khalid Aucho, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Shaban Djuma, David Bryson, Dickson Ambundo na Yusuph Athumani.

 

Wakikamilisha usajili huo, Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa wachezaji wawili Yannick Bangala Litombo ambaye tayari amesitisha mkataba wa kuichezea klabu ya Far Rabbat ya nchini Morocco na Jesus Moloko anayeichezea AS Vita ya Congo, Kishansa.

Yanga ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Moloko kwa atakayekuja kuchukua nafasi ya kiungo mshambuliaji Tuisila Kisinda aliyetimkia Berkane ya nchini Morocco Championi Jumatano, linakuletea mifumo mitatu itakayombeba Nabi katika msimu ujao akitumia ambayo ni 4-4-2, 4-5-2 na 4-1-3-2.Akitumia mfumo wa 4-4-2, Nabi atawatumia wachezaji hawa kipa, Diarra, Shabani Djuma, David Bryson, Litombo, Dickson Job, Mukoko Tonombe, Moloko, Aucho, Makambo, Mayele na Yacouba Songne.

 

Mfumo wa 4-5-2, Nabi atatakiwa kutumia kikosi cha wachezaji hawa nao ni kipa, Diarra, Djuma, Bryson, Litombo, Job, Aucho, Moloko, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Makambo, Yacouba na Ambundo.

Akitumia mfumo wa 4-1-3-2, ni kati ya mfumo mgumu ambao unahitaji viungo wenye kasi na uwezo wa kumiliki mpira muda mrefu huku wakiwapigia pasi za mwisho washambuliaji.

 

Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa hivi; kipa Diarra, Djuma, Bryson, Litombo, Mwamnyeto, Tonombe, Moloko, Aucho, Mayele, Fei Toto na Yacouba.Fei Toto ameingia kucheza namba kumi katika kikosi hicho maalum kwa ajili ya kumchezesha Mayele akipokea mipira kutoka kwa Aucho na Makambo na hiyo ndiyo nafasi aliyokuwa akichezeshwa na Nabi katika msimu uliopita.

 


WATAMBA KUWEKA
REKODI

Usajili mzito ambao unaendelea kufanywa na uongozi wa Yanga umezidi kuwapa jeuri, ambapo sasa wameweka wazi kuwa wanataka kuweka rekodi ya kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro alisema: “Kikosi chetu kinaendelea kufanya usajili mkubwa kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, tayari tumewatambulisha rasmi baadhi ya wachezaji na kuna majembe zaidi yanakuja.

 

“Malengo yetu ni kufanya vizuri msimu ujao kwenye michuano mbalimbali tutakayoshiriki, lakini malengo yetu makubwa zaidi ni michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo tunataka kuandika rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na timu za Tanzania.”

STORI: WILBERT MOLANDI NA JOEL THOMAS

Leave a Comment