×

Ndugai Atoa Tamko Wabunge Ambao Hawajaapa

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemWapisha Prof. Shukrani Manya kuwa mbunge rasmi huku akitoa wito kwa wabunge wa ACT Wazalendo kutoa taarifa ili wapangiwe kuja kuapishwa na kuwatumika wananchi.

 

Akizungumza baada ya kiapo cha Manya jijini Dodoma leo, Ndugai amempongeza mbunge huyo kwa kuteuliwa kuwa mbunge huku akisema bunge hilo haLitaki kurudisha nyuma kasi ya serikali.

 

“Nitoe wito kwa wabunge wengine wowote wale, kumbukumbu zangu zinaonyesha kuna wabunge wanne wa ACT Wazalendo ambao bado hawajaapa ningetoa wito kama wenyewe wakiwa tayari kutumikia nchi yao kama kweli waliomba ubunge kutumikia wananchi, hawana sababu ya kuzurura huko walipo watoe taarifa kwa spika haraka tuwapangie ili wapate kiapo waweze kufanya kazi ya mbunge,” amesema Ndugai.

 

Uapisho wa Prof. Shukrani Manya unakuja  baada ya uteuzi wa rais uliofanyika leo  Desemba 11, 2020, ambapo amemteua kuwa Naibu Waziri wa Madini na Mbunge mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Leave a Comment